Hii leo Eatv imepita katika mitaa mbali mbali ya jiji kuzungumza na makundi mbalimbali ya watu wakiwemo watumishi pamoja na wajasiriamali kujua kwa namna gani jamii inauelewa juu ya masuala ya hisa ambapo wengi kati yao wameelezea suala la elimu ni changamoto kubwa.
"Mimi nachokifahamu ni zile hisa ambazo huwa tunaziinunua kwenye vikundi vya vikoba huku mitaani kwetu zinatusaidia Sana lakini hizi hisa nyingine bado sijajua nazipataje na ntapataje faida" Consolata Mgata"-Mkazi wa Kipawa.
Aidha baadhi ya kina mama wamesema wao wamekuwa wakitumia ununuzi wa hisa jamii katika baadhi ya vikundi vyao mitaani na vimekuwa vikiwasaidia Eatv ikaenda mbali zaidi kwa kuzungumza na mmoja ya mama Bi Stella Katenga. ambaye amestaafu kwa sasa akielezea uthubutu aliiwahi kufanya katika uwekezaji wa hisa.
" Kiukweli ndugu mwandishi mimi niliwahi kununua hisa kwa kampuni Moja hivi hapa mjini nashukuru mungu kwa Sasa Kuna gawio napata kipindi hiki nikuwa nimestaafu labda niseme tuu jamii inapaswa kubadili fikra sio mpaka wote tufanye biashara za kuuza Nyanya".alisema bi Stella Katenga -Muuguzi Mstaafu Hospitali ya Muhimbili.
Kwa Sasa serikali imekuwa ikiwawezesha wanawake vijana na watu wenye ulemavu Ambapo elimu hii ya uwekezaji katika hisa bado elimu hii imeombwa kutolewa ili kwa wasioweza kufanya biashara wawekeze fedha ili kupata faida za mwishoni mwa mwaka.