Ijumaa , 28th Aug , 2020

Mara baada ya kuanza kwa kampeni za vyama vya Siasa hii leo Jeshi la zimamoto na uokoaji limewataka wananchi kuhakikisha wanachukua tahadhari zote za kudhibiti vyanzo vya moto.

Mojawapo ya magari ambayo hutumiwa na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji

Nakusisitiza umuhimu wa  kupeana zamu kwenda kwenye mikutano ya kampeni ili kuhakikisha nyumbani anabaki mtu mwenye uelewa wa kutoa taarifa endapo itatokea janga la moto.

Akizungumza na EATV Mkaguzi Michael Bachubira ambaye pia ni Afisa oparesheni Mkoa wa kizimamoto Moto Temeke amesema mara nyingi uzoefu umeonyesha kuwa kipindi Cha kampeni kumekuwepo na mihemuko hususani kwa wakereketwa hali ambayo katika masuala ya maokozi Jeshi limetoa Tahadhari wananchi familia kuchukua tahadhari kubwa.

Aidha ameitaka jamii kuacha Ile dhana kwamba mara baada ya wananchi kuiripoti Gari huwa inaondoka bila maji Huku akielezea utayari wa Jeshi hilo hasa katika kipindi hiki cha uchaguzi ili kuhakikisha jamii inakuwa salama.