Makamu Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Mkuu Mstaafu wa Zanzibar mheshimiwa Hamid Mahamoud Hamid, amesema hayo leo wakati akitangaza kukamilika kwa maandalizi ya uboreshaji wa daftari hilo, zoezi litakaloanza mwezi Novemba mwaka huu.
Kwa mujibu wa Jaji Hamid, uboreshaji wa daftari hilo umechelewa kwa takribani miezi miwili kutokana na kukosekana kwa fedha, ambapo amesema serikali imeipatia tume hiyo fedha za awali shilingi bilioni 15, ingawa hata hivyo hakuwa tayari kusema kiwango halisi cha fedha kinachohitajika kugharamia zoezi hilo.
Zoezi hilo limekuwa likitolewa matamko tofauti ambapo hivi karibuni Mwanasheria mkuu wa Serikali Jaji Fredrick Werema alisema kura hiyo itapigwa March 31 lakini Rais wa Jamhuri wa Muungano Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akasema zoezi hili litafanyika kuanzia Mwanzoni mwa mwezi wa nne.