Jumatatu , 15th Jun , 2020

Wachezaji na viongozi wa Yanga leo Juni 15, 2020 wamefika Bungeni Dodoma wakitokea Shinyanga baada ya mchezo wa Ligi kuu dhidi ya Mwadui FC uliopigwa Jumamosi na Yanga kushinda goli 1-0. 

Wachezaji wa Yanga wakiwa katika Jengo la Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Dodoma.

Spika Job Ndugai amewakaribisha na kuwatambulisha na wabunge wakawashangilia huku wakimulizia Bernard Morrison ambaye hajaambatana na timu.

Spika amewapongeza Yanga wa ushindi dhidi ya Simba Machi 8, 2020 ambapo pia akawaomba wabunge wa Simba wawapigie makofi wachezaji na viongozi wa Yanga waliofika Bungeni hapo.

Zaidi msikilize Spika hapo chini