Kiongozi huyo wa genge Khalil Subjee, ambaye anajulikana kama Jenerali, amesema ataagiza kuuawa mwanariadha huyo, iwapo umaarufu wake utamfanya asipate wakati mgumu gerezani.
Wakili anayemtetea mwanariadha huyo Barry Roux amenukuu habari iliyoandikwa kwenye gazeti moja na kusema kuwa maisha ya Pistorius yatakuwa hatarini iwapo atafungwa jela kwa kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp.
Roux amesema Subjee, anayeongoza magenge 26 ya uhalifu na anayehofiwa mno amedai yeye ni kiongozi wa gereza na kutoa vitisho dhidi ya Pistorius katika mahojiano aliyoyafanya kwa njia ya simu akiwa gerezani.