
Mkuu wa Wilaya ya Nyang'wale Mkoa wa Geita, Hamim Buzohera Gwiyama
Taarifa ya msiba huo imetolewa na Waziri wa Nchi - TAMISEMI Selemani Jafo.
Marehemu Hamim Buzohera Gwiyama aliteuliwa na Rais John Magufuli Juni 26, 2016 kuwa mkuu wa Wilaya ya Nyang'wale.
Aidha Waziri wa Nchi - TAMISEMI Selemani Jafo ametoa pole wa familia na ndugu na kueleza taarifa zaidi kuhusu mazishi zitatolewa na Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Geita.