Alhamisi , 9th Oct , 2014

Staa wa muziki Mkata Mkaa Chegge Chigunda amesema kuwa, tokea ameanza kufanya muziki ngoma zake tatu, Uswazi Take Away, Twende Zetu na Karibu Kiumeni ndio kazi ambazo anazikubali zaidi kuliko rekodi nyingine zote.

msanii wa muziki nchini Tanzania Chegge Chigunda

Chegge amesema kuwa, kwa upande wake kama msanii anafurahia sana anapozisikiliza rekodi hizo, akiendelea mbele zaidi kusema kuwa ngoma ya Uswazi Take Away imeingia katika orodha hiyo ikiwa ni kazi ambayo melodi na tungo zake zilimjia akiwa tayari ameshaingia booth kurekodi.