
Mshukiwa akiwa katika vipimo
Kwa mujibu wa mtandao wa Kenyan, mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 54, alijifungia katika hoteli moja mjini Machakos akihofia kuwa na virusi vya Corona, baada ya majirani kulalamika juu ya tukio hilo na polisi kuchukua hatua ya kumkamata.
Afisa wa afya katika Mji wa Machakos, Ancent Kituku amethibitisha kuwa mshukiwa huyo pamoja pamoja na mwongozaji watalii aliyeambatana naye walipimwa na maafisa wa afya, ambapo hawakukutwa na virusi hivyo.
Hali hiyo inatokea baada ya tahadhari kubwa nchini humo kufuatia kupatikana kwa watu watatu wenye virusi hivyo, wawili kati yao wamegundulika baada ya kugusana na mgonjwa wa kwanza.