
Droo ya hatua ya 16 bora UEFA
Kwa Upande wa Liverpool ambao waliongoza kwa kukusanya alama kwenye hatua ya ligi wao watavaana na matajiri wa Ufaransa PSG, huku Barcelona ikipangwa kuvaana na Benfica ya Ureno
Kwa upande wa wababe wa Italy Inter Milan wao wamepangwa kucheza na Feyenoord, Borussia Dortmund watacheza na Lille, wakati Club Brugge akivaana na Aston Villa
Miamba ya Ujerumani Bayern Munich wao watacheza na bingwa mtetezi wa Bundesliga Bayer Leverkusen na Mechi nyingine PSV watakabiliana na Arsenal