Ijumaa , 28th Feb , 2020

Mkuu wa Wilaya ya Chato Mhandisi Charles Kabeho, amewapa adhabu wakazi wa Kata ya Buziku wilayani humo ya kufyeka na kuteketeza bangi ambayo wameilima kwenye eneo walilopewa na Serikali kwa ajili kilimo cha mazao.

Mmea wa Bangi.

Mhandisi Kabeho amesema kuwa eneo hilo walilogawiwa wananchi ni sehemu ya Ardhi ya Hifadhi ya Msitu wa Biharamulo na kwamba watakapokiuka tena basi wataondolewa katika eneo hilo.

"Ndio maana nimewachukua wao wenyewe wang'oe bangi zao ili liweze kuwa fundisho kwao, maana haiwezekani mtu alime halafu wao wamuangalie na wangoje mimi na vyombo vyangu vya ulinzi na usalama kuja kuwasimamia" amesema Mhandisi Kabeho.