Alhamisi , 6th Mar , 2025

Mwanzoni mwa mwezi wa pili mwaka huu Bilionea Elon Musk alitoa ofa ya kuhitaji kununua kampuni ya OpenAI ambayo inaimiliki ChatGPT kwa kiasi cha zaidi ya shilingi Trilioni 256

 

Ila hapo kwenye Trilioni 256 siyo mwanzo wa sakata la Elon na ChatGPT, ukirudi nyuma mwaka 2015 wakati ChatGPT inaanzishwa miongoni mwa waanzilishi wake ni Sam Altman na Elon Musk lakini mwaka 2018 Elon Musk aliondoka kwenye kampuni hiyo.

Mwanzoni wakati ChatGPT inaanzishwa lengo lilikuwa ni iwe bure kwa wote na inufaishe jamii, mambo yalianza kwenda kombo baada ya kampuni hiyo kuhitaji pesa ili kujiendesha na kukuza zaidi mfumo huo wa akili unde.

Lakini kampuni haikuwa na pesa, Sam Altman na Greg Brockman ambao ni miongoni mwa waanzilishi walikuja na wazo la kutengeneza mfumo mpya wa ChatGPT ambao utawafanya watumiaji walipie ili kutumia mfumo huo, kitu ambacho hakikumpendeza Elon Musk na kuchukua maamuzi ya kwenda kuishtaki kampuni hiyo kwa kile alichodai kwamba wamekiuka dhima nzima ya kuanzishwa kwa kampuni hiyo.

Baada ya shtaka la Elon kufika mahakamani Jaji alitupilia mbali shtaka hilo na hakuona sababu ya zuio hili kitu ambacho kiliwafanya wakina Sam Altaman kushinda kesi na sasa huenda ChatGPT ikajiendesha kwa faida zaidi.