Jumapili , 2nd Feb , 2020

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene amesema Jeshi la Polisi linamshikilia Mtume na Nabii Boniface Mwamposa baada ya kutoroka mjini Moshi kufuatia vifo vya watu 20 ambao walikuwa wanakanyaga mafuta ya upako mahala alipokuwa akihubiri.

Waziri George Simbachawene na Mtume na Nabii Mwamposa

Tukio hilo limetokea jana, Februari 1, 2020 ambapo waumini hao walikuwa wakigombania kukanyaga 'maji ya upako' ya Mtume na Nabii Mwamposa katika Uwanja wa Majengo mjini  Moshi, mkoani Kilimanjaro.

Akizungumzia tukio hilo, Waziri Simbachawene amesema serikali inafikiria kutengeneza kanuni za uanzishwaji wa huduma za kiroho kuwa lazima mchungaji awe amesomea theolojia.

Mtume Mwamposa atapelekwa mjini Moshi kwa ajili ya kufunguliwa mashtaka.