Jumatano , 1st Oct , 2014

Mtayarishaji muziki, Lamar ambaye hivi karibuni amekuwa na session katika studio yake na msanii wa kimataifa Tumi Mole Kane ambaye ana project na msanii Chidi Benz na Vanessa Mdee pia, amezungumzia sanaa ya mkali huyo wa kimataifa.

mtayarishaji muziki nchini Tanzania Lamar

Lamar ambaye kazi hii ni moja ya kazi Kubwa kufanya akiwa na msanii kutoka nje ya mipaka ya hapa Bongo, amesema kuwa Tumi ni msanii ambaye anafanya kazi yake kwa umakini na kwa upande wake amekwishamaliza kutengeneza ngoma ambayo jamaa huyu ameifanya kushirikiana na wasani hawa wakali kutoka Bongo.