Rais Magufuli
Rais Magufuli ametoa kauli hiyo wakati akizungumza kwenye uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Mwanakwerekwe iliyopo visiwani Zanzibar.
Rais Magufuli amesema kuwa "Nasikitika sana wanapotangaza matokeo unakuta Shule za Zanzibar zinafuatana kuwa za mwisho hii ni aibu, viongozi mpige vita hii aibu, najua wengine hawawezi kuwaeleza mimi lazima nitawaeleza"
"Nasikitika sana wanapotangaza matokeo ya Sekondari unakuta Shule za Zanzibar zinafuatana kuwa za mwisho hii ni aibu, viongozi mpige vita hii aibu, najua wengine hawawezi kuwaeleza mimi lazima nitawaeleza." - Rais @MagufuliJP#JPMZanzibar pic.twitter.com/fLs6RgQmyD
— East Africa Radio (@earadiofm) January 11, 2020
Aidha Rais Magufuli ameongeza kuwa "Nataka mpaka Machi kabla ya tarehe 30, jengo hili wanafunzi wawe wanaingia ndani, hii hela inayotumika hapa ni hela ya Wanzanzibar na watailipa, nakuomba Mkandarasi ukamilishe kwa wakati, Katibu Mkuu marufuku kuwatetea Wakandarasi"
Kwa sasa Rais Magufuli yuko visiwani Zanzibar kwa ajili ziara ya kikazi ambapo kesho atashiriki Sherehe za miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar.


