
Waziri ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Selemani Jafo
Akizungumza mara baada ya agizo la Rais Magufuli alilolitoa jana akiwa njiani kuelekea Mwanza, ambapo Jafo ametoa wiki moja kuanzia leo hadi Jumatano ijayo apate taarifa ya Halmashauri zote zilizochukua mikopo, kutoka kwenye mabenki kwadhumuni gani na kiasi gani na riba yake ikoje.
Aidha Waziri Jafo hategemei Mkurugenzi yeyote kutoa taarifa za uongo na atakayetoa taarifa za uongo atachukuliwa hatua za kinidhamu.
Jafo amesema waliochukua na bado hawajaitumia wazirudishe kwenye mabenki walipokopa na kuanzia sasa kila kitu kisimame.