Rais Magufuli
Taarifa hiyo imetolewa leo Oktoba 19, 2019, na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Gerson Msigwa, ambapo nafasi ya Mkuu wa Wilaya imechukuliwa na Hashim Abdallah Komba.
Uteuzi mwingine ambao umefanywa na Rais Magufuli leo ni wa Godfrey Mweli, ambaye amekuwa Naibu katibu mkuu TAMISEMI, akichukua nafasi ya Mathias Kabunduguru ambaye amekuwa Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania.
Katika hatua nyingine Rais Magufuli amemteua Mathias Kabunduguru, kuwa mtendaji mkuu wa Mahakama ya Tanzania, akichukua nafasi ya Hussein Katanga ambaye ameteuliwa kuwa Balozi.




