Jumamosi , 10th Aug , 2019

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigela, ametoa wiki  tatu kwa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza kurudisha fedha za wananchi zilizochangishwa kwa muda wa miaka mitatu bila miradi kutekelezwa.

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigela.

Fedha hizo zilizochangwa na wananchi ni  kwa ajili ya kuchimba visima, ili kumaliza kero ya uhaba wa maji vijijini.

Ametoa agizo hilo leo Jumamosi Agosti 10, 2019, wakati wa ziara yake ya kata kwa kata wilayani humo kusikiliza kero za wananchi.

"Naagiza Halmashauri rudisheni fedha za wananchi ambazo kila kata mmechangisha laki tano na Kama mmezitumia mtazitapika" amesema Shigela.

Halmashauri ya Muheza iliingia mkataba na mwekezaji kwa ajili ya kuchimba visima katika vijiji vilivyopo  katika Wilaya hiyo kwa gharama ya shilingi laki tano, miradi ambayo hadi sasa haijatekelezwa.