
Wachezaji wa Simba wakifanya mazoezi
Akiongea kwenye 5SPORTS ya East Africa Television, Manara ameeleza kuwa kuna 'suprise' watu wajiandae kumjua kesho wakati akimtambulisha.
''Kuna mchezaji mpya kabisa na anacheza nafasi zote uwanjani, nitamtambulisha wa mwisho'', alisema Manara.
Manara pia ameongeza kuwa, tayari kocha Patrick Aussems ameshapewa malengo ya msimu ujao wa 2019/20, ambapo anatakiwa kuhakikisha timu inatetea ubingwa wa ligi kuu kisha kufika nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Simba leo wanaadhimisha tamasha lao la 'Simba Day' ambapo linafanyika kwa mara ya 10 mfululizo ikiwa ni maalum kwa shughuli mbalimbali ikiwemo kutambulisha wachezaji watakaowatumia msimu mzima.