
Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa Sisty Nyahoza
Naibu Msajili ameyabinisha hayo leo Julai 27, 2019, katika mkutano mkuu wa kuchagua viongozi wa chama hicho, ambapo amesema Serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Dkt. John Magufuli, inachukizwa na wapinzani wasiofuata kanuni na taratibu za nchi.
''Serikali ya awamu ya Tano haichukii upinzani ila inachopingana nacho ni wapinzani na mpinzani ni yule anayefuata sheria na kanuni na anayesimamia maadili ya nchi kama huyu James Mbatia na ni M/kiti wa chama cha upinzani na sio wapinzani, ameweka pembeni chuki, bughudha, matusi na kila jambo linaloleta mtafaruku''. Amesema Nyahoza.
Aidha Nyahoza amesema yeye kama Naibu msajili, anakiona chama cha NSSR Mageuzi ndio chama cha kuigwa na vyama vingine na kwamba anaiona safari nzuri ya chama hicho.
''Chama cha NSSR Mageuzi ni chama cha mageuzi kwa sababu mumeendelea kutii sheria za nchi kama zinavyoelekezwa hii inathibitisha kwamba nyinyi ni baba wa mageuzi na mimi kama Naibu msajili wa vyama, naunga mkono kabisa mwenendo wa NSSR Mgeuzi katika nchi hii''. Ameongeza.