Jumapili , 21st Jul , 2019

Mzalishaji 'producer' mkali wa ngoma za Bongo Fleva ambaye pia ni msanii, Mr. T Touch amejibu tetesi kuhusu kupewa pesa za kupangisha studio yake maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam.

Mr. T Touch

Producer huyo ambaye anamiliki studio ya Touch Sound, kupitia Friday Night Live (FNL) amesema kuwa katika mafanikio ya studio yake hakuna mkono wa mtu yeyote na kama yupo basi ajitokeze aende ofisini kwake.

"Kwanza Touch Sound haina mkono wa mtu yeyote, mimi ndiye CEO. Mtu akikuambia ana mchango pale hebu mlete kwangu. Huwa ninabadilisha mahali kwa sababu ninataka kubadilisha kila kitu, nikifanya kazi mwaka mmoja sehemu moja lazima nibadilishe ili niwe mpya na nipate vitu vipya", amesema.

"Huwa ninashindwa kufanya kazi sehemu moja muda mrefu, labda nibadilishe muonekano wa studio yangu", ameongeza.

Mr. T Touch hivi sasa ameamua kujikita katika kuimba na wiki hii ameachia ngoma yake mpya ya 'Simu moja' aliyofanya na Billnass. Ngoma hiyo ni ya tatu kwa T Touch baada ya kuamua kujikita rasmi katika kuimba.