
Obrey Chirwa
Meneja wa klabu ya Azam FC, Philip Alando amesema kuwa taarifa hizo hazina ukweli wowote kwa sababu makubaliano ya klabu na mchezaji huyo ni kufanya mazungumzo mara baada ya mkataba kumalizika.
"Lazima tuheshimu makubaliano na siku zote tumekuwa katika misingi hiyo, mfano hivi karibuni kulikuwa na taarifa kuwa Yakuby anakwenda Simba lakini mwisho wa siku akasaini hadharani na Azam FC na kila mtu aliona", amesema Alando.
"Dirisha dogo tuliingiza wachezaji wawili wa kigeni, Chirwa na Stephen Kingu Mpondo lakini sioni mtu akimuulizia. Pia mkumbuke usajili haufanywi na uongozi, usajili unafanywa na makocha halafu viongozi kazi yao ni kukamilisha tu", ameongeza.
Siku za karibuni zilienea taarifa kuwa Obrey Chirwa amegoma kusaini mkataba mpya na klabu hiyo huku zikieleza zaidi kuwa yuko mbioni kujiunga na mabingwa wateule wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba.