Ijumaa , 26th Apr , 2019

Hii leo, April 26, 2019, msanii wa Bongo Fleva, Alikiba ameachia wimbo mpya aliouita jina la 'Mbio'.

Alikiba

Muda mfupi baada ya kuachia wimbo huo, Alikiba ameeleza siri nzito iliyopelekea kuachia wimbo huo hivi sasa.

Katika ukurasa wake wa Twitter, Alikiba amesema kuwa wimbo huo aliuandika takribani miaka 10 iliyopita aliposafiri kwa mara ya kwanza nchini Oman.

Mara ya mwisho kwa Alikiba kutoa wimbo wa peke yake ni takribani miezi minne iliyopita ambapo alitoa wimbo wa Kadogo.