Mashabiki wa Simba
Simba ambayo imetoka asubuhi ya leo jijini Dar es salaam na kuwasili Morogoro majira ya mchana, imepokelewa na mamia ya mashabiki katika hoteli waliyofikia ambao muda wote wameonekana kutaja majina ya wachezaji.
Jina la mshambuliaji John Bocco ndilo lilliloibua shangwe kubwa zaidi baada ya kushuka kutoka kwenye basi, ikionesha kuwa mashabiki wamekubali kiwango alichokionesha katika mechi mbili kubwa na muhimu za mwisho.
Mechi hizo ni ili iliyoipeleka Simba robo fainali ya Klabu Bingwa Afrika baada ya kuifunga AS Vita mabao 2-1 katika Uwanja wa Taifa pamoja na mechi iliyoipeleka Taifa Stars kwenye fainali za AFCON kwa kuichapa Uganda kwa mabao 3-0, ambapo katika mechi zote mshambuliaji huyo ameonesha kiwango kikubwa.
Makamanda wetu walivyopokelewa mji kasoro bahari (Morogoro). Siku ya Jumapili watakuwa uwanja wa Jamhuri kuwapa burudani Wanasimba wote. #NguvuMoja pic.twitter.com/ziQwF7cSni
— Simba Sports Club (@SimbaSCTanzania) March 29, 2019
Mabingwa hao watetezi wa ligi kuu wanatarajia kupambana na Mbao FC katika Uwanja wa Jamhuri kutokana na Uwanja wa Taifa kuwa katika maandalizi ya michezo ya AFCON ya vijana chini ya miaka 17 inayoratajia kuanza mwezi ujao nchini Tanzania.
Nafasi ya Simba katika msimamo wa ligi
Katika msimamo wa Ligi Kuu, Simba inakamata nafasi ya tatu ikiwa na pointi 54 baada ya kushuka dimbani michezo 21 huku Mbao FC ikiwa katika nafasi ya 14 kwa pointi 36 baada ya kushuka dimbani michezo 30.
Bonyeza hapa chini kutazama zaidi.