Khalifa ametoa kauli hiyo jijini Dar es salaam wakati akizungumza na www.eatv.tv juu hatma ya Wabunge ambao walionekana kutounga mkono upande wa Prof Lipumba, wakati mgogoro wa chama hicho ukiendelea.
"Katika mahojiano yangu yote yale, tumesema Wabunge hatuna shida nao yoyote ile, ila tumesema tutawaita kama Wabunge ili waje kutoa ushirikiano," amesema Khalifa.
"Kuhusu Mbunge Katani ambaye alionekana kuwa sio upande wetu hatumfyeki, nachokiamini Katani atatoa ushirikiano, kama anaamini aliingia katika chama ili asipate uongozi basi tunamruhusu kuandika barua ya kujiuzulu Ubunge." ameongeza Khalifa.
Hivi karibuni Khalifa huyo akizungumza na www.eatv.tv alibainisha kuwa chama hicho kipo tayari kushirikiana na vyama vingine ikiwemo Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa ajili ya kujenga demokrasia Tanzania.





