Alhamisi , 6th Mar , 2014

Nchi za Afrika Mashariki zipo hatarini kuzuiwa kufanya biashara na Marekani iwapo hazitatumia mfu

Nchi za Afrika Mashariki zipo hatarini kuzuiwa kufanya biashara na Marekani iwapo hazitatumia mfumo na sheria za Marekani katika kukabiliana na fedha haramu na uhalifu katika sekta ya fedha.

Mshauri wa masuala ya fedha kutoka taasisi ya Deloitte Bw. Robert Nyamu, ameyasema hayo jijini Dar es Salaam leo, wakati akitoa ripoti ya hali ya uhalifu katika sekta ya fedha kwa nchi za Afrika Mashariki, ambapo Tanzania imeonekana kuongoza kwa wizi wa fedha unaofanywa kwa njia ya unyang'anyi.

Nyamu amefafanua kuwa Marekani imepitisha sheria ijulikanayo kama Foreign Accounts and Tax Compliance Act au kwa kifupi FATCA, ili kudhibiti ukwepaji kodi na fedha haramu ambapo nchi za Afrika Mashariki zitatakiwa kuweka bayana taaria za akaunti za wateja wanaotuma na kupokea pesa kutoka Marekani.