Jumatatu , 11th Feb , 2019

Mchekeshaji maarufu bongo, Mc Pilipili ameweka wazi kwamba anaweza akalia siku ya harusi yake kama alivyofanya siku ya kuchumbia, kwani yeye hana uvumilivu na hawezi kuzuia hisia kama wanaume wengine.

Mc Pilipili amefunguka hayo akihojiwa na EATV na kusema kwamba yeye yuko 'real', hivyo hawezi kujikaza kiume kama wengi wanavyomtaka awe na kutotumia vibaya machozi yake.

Mimi nilikuwa nalia na huwezi kusema matumizi mabaya ya machozi kwa mtoto kama yule, siku ya harusi naweza nikajisikia kulia, mimi sina zile za kiume, we mwanaume jikaze, nakuwa real na hisia zangu, naangua kilio fresh, najua kuwa real, hata siku ya harusi naangua kilio fresh tu, nakuwa real”, amesema MC Pilipili.

Hata hivyo Mc Pili Pili ambaye jina lake halisi Emmanuel Mathias, amedai kwamba watu wanaomkebehi kuhusu kulia hawamuumizi kichwa, kwani ndivyo alivyo anapokuwa na hisia.