Alhamisi , 19th Feb , 2015

Star wa muziki Mike Tee, ameelezea uwezo na nafasi mpya ambayo amejitengenezea katika gemu ya burudani, ambapo sasa pia amejikita katika kufanya utafiti wa kile mashabiki wanachokitaka.

Mike Tee

utafiti huo umeegemea zaidi katika kazi za wasanii hususan video kutoka mtaani, na kuwapelekea wasanii hao mawazo haya kwa ajili ya kuyatumia.

Mike amesema kuwa, anafanya hivyo kutokana na kukaa muda mrefu katika mitaa na kusoma kile ambacho kinatakikana, na hii ni katika kusaidia kuzalisha kazi za wasanii katika muundo ambao mashabiki wanautaka na hivyo kuzileta pande hizo mbili karibu zaidi.

Tags: