
Mwana FA
Mwana FA ameyasema hayo baada ya kejeli za mashabiki wa Yanga kuzidi ambapo ametaka wakutane ili kuwaweka sawa.
"Ndugu zangu TFF, kwa hisani yenu msiahirishe mechi ya tarehe 16 kwa sababu yeyote ile iliyo ndani ya uwezo wa kibinadamu, kuna maneno yametukera tunataka tuwekane sawa. Ahsanteni".
Mechi ya marudio ya Simba na Yanga inatarajiwa kuchezwa Februari 16 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.