Jumatano , 9th Jan , 2019

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi, Humphrey Polepole amekosoa maandamano mbalimbali ambayo yamekuwa yakilenga kuwapongeza baadhi ya viongozi wa nchi kwa kile alichokidai kuwa huenda yakaleta machafuko kwa baadhi ya waandamanaji.

Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi, Humphrey Polepole

Polepole ametoa kauli hiyo wakati akizungumza kwenye kipindi cha East Africa Breakfast cha EA Radio akijibu swali juu ya utata wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi UVCCM, kupewa kibali cha kuandamana huku vijana wa chama cha ACT - Wazalendo wakipigwa marufuku.

"UVCCM kupewa kibali cha kufanya maandamano Kigoma kulifuata utaratibu ambao haukuwa na madhara na wao ndiyo walioanza, endapo tungeruhusu wote na kukutana barabarani unadhani nini kingetokea. Mimi ni mhanga wa matukio hayo naelewa", amesema Polepole.

"Maandamano ambayo hayana faida wala kusaidia kupeleka mkono kinywani, hayana tija, maandano ya vijana wa ACT-wazalendo kule Kigoma walikuwa wanataka kumpongeza mtu ambaye hayupo huko", ameongeza Polepole.

Aidha Polepole azmezungumzia kuhusiana na Katibu Mkuu wa CCM kuonekana kupewa kingo'ora cha polisi ikiwa tofauti na viongozi wengine wa upinzani amesema, "Dkt. Bashiru kupewa 'Escort' ya Jeshi la Polisi ni utaratibu wa kawaida ambao tuliomba kama chama kwa kufuata utaratibu wala hakuna upendeleo kama ukifuata utaratibu unavyotaka".