
Mbunge wa Geita Vijijini Musukuma
Akiongea katika mkutano wa hadhara katika moja ya ziara zake, Musukuma amesema haiwezekani yeye kama mbunge akashiriki kwenye kuvunja sheria hivyo kwa kuwa taratibu za kumfukuza hazijafuata sheria ni lazima arudi ofisini na aendelee na kazi.
''Mimi sipingani, kama anakwamisha maendeleo na sipingani kama amefukuzwa na chama ni haki yao lakini ni lazima wapeleke barua kwa Mtendaji ambaye anapeleka kwa DAS kisha mkuu wa Wilaya ataitisha kikao kwenye kijiji na kutangaza kumvua uongozi vinginevyo wewe bado ni Mwenyekiti'', amesema.
Mwenyekiti huyo wa Kitongoji alikuwa amesimamishwa uongozi pamoja na kuvuliwa uanachama na kamati ya siasa ya tawi na Kata, kwa tuhuma za kukwamisha shughuli za maendeleo.
Aidha Musukuma ameeleza kuwa yeye pia amewahi kuwa mhanga wa tatizo la hilo ambapo mwaka 2001 alivuliwa Uenyekiti wa Halmashauri baada ya kuwabana wazungu wenye migodi pamoja na viongozi waliokuwa wanashirikiana nao.
Musukuma pia ameshangazwa na uongozi wa Kata hiyo, kuvifungia ofisini vifaa vya ujenzi wa kituo cha polisi cha kata hiyo, kwa zaidi ya miaka mitano, ikiwemo mabati na mifuko ya saruji ambayo imeanza kuharibika, na kuahidi kuchangia vifaa vilivyobaki ili kukamilisha ujenzi huo.
Tazama Video hapo chini