
Mbwana Samatta
Samatta ambaye alianza katika kikosi cha jana, alicheza kwa dakika zote 90 za mchezo licha ya kutofunga bao lolote.
Kwa matokeo hayo, Genk inaendelea kuongoza ligi ya Ubelgiji ikifikisha pointi 35 baada ya kutoka sare mechi tano kati ya mechi 15 ilizocheza, nyingine zote 10 ikishinda. Ambapo sasa inafuatiwa na Club Brugge yenye pointi 31 katika mechi 15 pia na sawa na Antwerp.
Kwa ujumla Samatta jana amefikisha mechi 129 katika mashindano yote tangu amejiunga na Genk Januari mwaka 2016 akitokea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na amefunga jumla ya mabao 51.
Katika Ligi ya Ubelgiji pekee amefikisha mechi 100 na kufunga mabao 36, Kombe la Ubelgiji mechi nane mabao mawili na Europa League mechi 21 mabao 14.