
Katibu mtendaji wa Baraza la mitihani la taifa, Dkt. Charles Msonde.
Mitihani hiyo itaanza Novemba 12 hadi 23 2018, ambapo wavulana ni 261,159 sawa na asilimia 47.93 huku wasichana wakiwa 283,707 sawa na asilimia 52.07.
Akizungumza na wanahabari Katibu mtendaji wa Baraza la mitihani la taifa, Dkt. Charles Msonde amesema kuwa mwaka huu kumekuwa na ongezeko la watahiniwa 23,011sawa na asilimia 4.41 ukilinganisha na mwaka 2017 ambao walikuwa 521,855.
"Mitihani ya kidato cha pili ni muhimu kwa wanafunzi na jamii kwakuwa tunapima uwezo na uelewa wa Wanafunzi katika yale waliyojifunza kwa miaka miwili", amesema Dkt. Msonde.
Dkt. Msonde amesema tayari maandalizi yamekamilika ikiwemo usambazaji wa mitihani katika vituo vya mitihani.