Jumamosi , 10th Nov , 2018

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Abdul Nondo, amefichua sababu ya yeye kutokwa na chozi baada ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Iringa , kuamuru kuachiliwa huru kwa makosa yaliyomkabili.

Abdul Nondo.

Mapema wiki hii Mahakama ya Hakimu Mkazi Iringa iliamuachilia huru Mwanafunzi huyo wa zamani ambaye alikuwa anasoma Chuo Kikuu Cha Dar es salaam baada ya kushtakiwa kwa makosa mawili ikiwemo kutoa taarifa za uongo pamoja na kudanganya kutekwa.

Akizungumza www.eatv.tv  Abdul Nondo amesema “nililia kwa sababu nilikuwa kwenye kipindi kigumu sana, sababu jamii ilikuwa inaniona mimi ni mhalifu wengine waliniona mwema, na  ndo maana unaona nimekonda sana.”

“Sheria ya chuo ilikuwa inanitesa sana, mimi sio muoga kuna vitu ambavyo lazima uwe na hofu navyo, mimi leo nisipokuwa na digrii watu hawawezi kuniamini, ila huwa sifikiri nikitoa tamko.” Amesema Nondo.

“Mimi sikuumbwa kuwa mbinafsi ndiyo maana tulikuwa tunawatetea wanafunzi mara kwa mara na nilikuwa nikiwasiliana na Waziri wa elimu Joyce Ndalichako, ili kuwasaidia wanafunzi waondokane na matatizo yao.” Ameongeza Nondo.

 

Kutazama mahojiano ya Abdul Nondo na www.eatv.tv bonyeza link hapa chini