Jumatano , 7th Nov , 2018

Mbunge wa Jimbo la Kaliua, Magdalena Sakaya amehoji hatua magari ya serikali kuonekana kwenye matukio mbalimbali ya ajali nchini ambayo yamekuwa yakisababisha vifo vya baadhi ya watumishi.

Magdalena Sakaya

Akiulizwa swali lake kwenye mkutano wa 13 kikao cha pili cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Sakaya alihoji iwapo sheria ya usalama barabarani haiwahusu magari ya serikali, kwa maana magari hayo hayazifuati sharia hizo.

Ajali zinazoongoza ni magari ya serikali kunakosababishwa na mwendokasi wa madereva ambao wanalazimishwa na mabosi wao na huwa hawasimamishwi popote kwani sheria za barabarani haziwahusu magari ya serikali?”, ameuliza Sakaya.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Massauni baada ya kushukuru mbunge huyo kwa swali lake, amesema kuwa kufuata sheria za barabarani hakubagui kwani kila mtu anatakiwa kuzifuata.

Kwanza nimshukuru Mbunge Sakaya kwa kuguswa na ajali za magari ya serikali lakini nimuhakikishie tu kila mtu anapaswa kufuata sheria za barabarani”,  amejibu Naibu Waziri Hamad Massauni.

Hivi karubuni katika Mkoa wa Singida, zaidi ya watumishi watano wa Wizara ya Kilimo walifariki dunia wakielekea kwenye shughuli za kikazi na mwezi huohuo mkoani Dodoma kupitia kamanda wa polisi, Giles Muroto alithibitisha kifo watu 7 waliokuwa watumishi wa serikali mkoani humo ambao walikuwa wakisafiri usiku