Jumapili , 4th Nov , 2018

Mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania bara (TPL), Simba inatarajia kufanya uchaguzi mkuu wa klabu hiyo kwa kuwachagua viongozi mbalimbali huku ikitangaza kutenga bajeti mpya itakayotumika katika kipindi cha mwezi  Julai 2018 hadi Juni 2019.

Simba

Katika kipindi hicho, Simba imetangaza bajeti ya jumla Sh 6.3 bilioni ambapo kati ya bajeti hiyo Sh 4.9 ikitoka katika vyanzo vya mapato vya klabu.

Pia katika taarifa hiyo ya klabu katika mkutano mkuu, Simba itakuwa na hasara ya jumla ya Sh 1.3 bilioni katika bajeti yake hiyo hadi Juni mwakani.

Mamia ya wanachama wa Simba wamejitokeza katika ukumbi wa JNICC jijini Dar es salaam, ambapo mkutano wake umeanza saa 3:55, ukiwa na ajenda mbili, ya kwanza ikiwa ni kusomwa na kupitisha taarifa mbalimbali za klabu na ajenda ya pili ikiwa ni ya uchaguzi mkuu wa klabu.