
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Simanjiro, Yefred Myenzi akimkabidhi fomu James Ole Millya.
Akizungumza na wanahabari mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Simanjiro, Yefred Myenzi amesema hadi jana saa 10 jioni hakuna mgombea aliyerudisha fomu zaidi ya mgombea wa CCM, James Millya.
"Kutokana na wagombea wengine kutorejesha fomu ,Millya amepita bila kupingwa na ndiye mbunge mteule anayesubiri kuapishwa", amesema Mnyenzi.
Naye mkurugenzi wa mji wa Babati, Fortunatus Fwema amesema mgombea ubunge wa Babati Mjini kwa tiketi ya CCM, Pauline Gekul amekosa mpinzani.
Amesema mgombea wa NRA, Feruzi Juma alichukua fomu lakini hakuirejesha huku mgombea wa CUF, Abubakari Peter fomu yake kubainika kuwa na kasoro.
Mkundi, Gekul na Millya walikuwa wabunge wa majimbo hayo kwa tiketi ya CHADEMA lakini walijiuzulu na kuhamia CCM.