Ijumaa , 2nd Nov , 2018

Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini amewataka wabunge kuandaa mkutano maalum utakaojadili masuala mbalimbali yanayohusu nchi kwa sasa kwa kile alichokidai kuwa hiyo ni haki yao ya kisiasa.

Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Arusha Godbless Lema ambaye pia ni Waziri kivuli wa mambo ya ndani nchi, amesema ataitisha mkutano wa dharula utakaohusisha wabunge ili kujadili mambo mbalimbali.

Katika mkutano huo, Lema amependekeza kuanzishwa kwa tume huru ya uchunguzi kwa ili kuchunguza taarifa ya mauaji iliyotolewa na jeshi la polisi kuleta mkanganyiko dhidi ya taarifa iliyotolewa na mbunge Zitto Kabwe.

Mkutano wa dharula uitwe Dar es salaam au Dodoma, na wabunge wote tukutane ili tutafute njia sahihi ya kupigania haki zetu za mikutano, na hatawakizuia ila iwe chanzo cha kuheshimu katiba. Hatuwezi kuendelea kuishi hivi.” Amesema Lema

Zitto amesema watu waliokufa ni wengi, idadi ya watu waliokufa ndiyo kinachopingwa nachopendekeza kiwepo chombo cha mbadala cha uchunguzi ili ijulikane nani mkweli kati ya  Zitto, Polisi au Mbunge wa jimbo lile Mheshimiwa Milima.” Amesema Lema

Leo Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe amefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa makosa matatu ya uchochezi, ambapo aliachiwa kwa dhamana na kesi yake itasikilzwa novemba 12 mwaka huu.