
James Harden
Rockets mpaka sasa wamefanikiwa kushinda mechi 1 tu kati ya 5 walizocheza huku wakipoteza 4 hivyo kuwa na mwanzo mbaya. Leo pia wanakabiliwa na kibarua kigumu dhidi ya Portland Trail Blazers mchezo ambao utarushwa na EATV pamoja na TV1.
Kwa upande wao Portland Trail Blazers wakiwa na nyota wao Damian Lillard wamecheza mechi 6 na kushinda 5 wakipoteza moja na leo watakuwa wenyeji wa Rockets.
Houston Rockets inakamata nafasi ya 14 kati ya timu 15 za upande wa Magharibi wakati Portland wakiwa katika nafasi ya 3.
Mchezo huo utapigwa usiku wa leo Jumanne, ambapo utaanza majira ya saa 9:00 usiku na kurushwa moja kwa moja kupitia EATV na TV1.