
Malimi Busungu
Mchezaji huyo hajaonekana katika kambi ya Lipuli Fc kwa zaidi ya wiki moja hivi sasa na taarifa za wapi hasa alikoelekea zikiwa hazijulikani.
Akithibitisha taarifa hiyo, Afisa Habari wa Lipuli FC, Clement Sanga amesema, " Ni kweli mshambuliaji wetu, Malimi Busungu hayupo kambini na sababu za kutokuwepo kambini sote kwa pamoja kama viongozi hatuzifahamu ".
"Nadhani ni zaidi ya wiki hivi hajaonekana kambini, hatujafuatilia kujua ni wapi alipo hadi hivi sasa kwasababu kwa sasa tumeweka macho yote katika mchezo wetu lakini kutokuwepo kwake uwanjani kutatuathiri kwa namna fulani", ameongeza Sanga.
Lipuli FC inacheza mchezo wake wa ligi kuu Tanzania bara jioni ya leo dhidi ya wenyeji Mbao FC katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza