
Aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini Lazaro Nyalandu.
Lazaro Nyalandu ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na www.eatv.tv iliyotaka kufahamu juu ya safari yake mpya ndani ya Chama hicho baada ya kukaa nje ya siasa za Tanzania kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Nyalandu amesema “safari hii sio kwa sababu ya mtu au mimi mwenyewe, ili taifa lifanikiwe, mimi kama sehemu ya sera za CHADEMA nitahakikisha ninaunganisha watu wa aina zote wanaotoka kwenye historia mbalimbali ya taifa kupitia ukuaji wa demokrasia nchini."
“Siasa ni watu ili tuweze kufanikiwa kama taifa, ni muhimu mimi kama Nyalandu mtu akinikosoa nakubaliana naye ila nitamuombea aishi maisha marefu ili ninapofanikiwa kwenye siasa za upinzani wajionee wenyewe." Ameongeza Nyalandu
Mwishoni mwaka jana kada huyo akiwa Mbunge wa Singida Kaskazini alitangaza kujivua nyadhifa zake ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kuomba ridhaa ya kujiunga CHADEMA kwa madai ya kukosekana kwa demokrasia ikiwa ni siku chache baada ya kurejea kutoka Nairobi Kenya kuzungumza na Mbunge wa Singida Mashariki Tundu lissu ambaye alishambuliwa kwa risasi.