Mmoja wa wachezaji wa mchezo wa chess akitafakari jambo wakati wa mchezo huo.
Wachezaji watano wa timu ya taifa ya mchezo wa chess ya Tanzania wanataraji kuondoka nchini kesho kuelekea nchini Norway ambako watashiriki michuano ya chess olimpiki itakayofanyika kwa siku 10 kuanzia August Mosi mwaka huu
Katibu mkuu wa chama cha chess Tanzania Nurdin Hasurj amesema michuano hiyo ni mikubwa ambayo huandaliwa na chama cha chess cha dunia FIDE na hufanyika kila baada ya miaka miwili
Aidha Nurdin amesema Tanzania itashiriki michuano hiyo ambayo itahusisha nchi 170 na wachezaji zaidi ya 2000 na ni kwa mara ya kwanza Tanzania kushiriki michuano hiyo mikubwa
Nurdin amesema pamoja na kushiriki michuano hiyo mikubwa kwa mara ya kwanza wana uhakika wa kufanya vema katika michuano hiyo kwakuwa wamefanya maandalizi ya kutosha kutokana na wachezaji wengi kucheza mashindano mengi ya ndani ambayo yalikuwa yakiandaliwa na chama cha chess Tanzania TCA.