Jumanne , 5th Jun , 2018

Anaitwa Yussuf Yurary Poulsen mwana wa ardhi ya Tanzania na Denmark, ambaye ni mcheza soka maarufu nchini Denmark, aliyetajwa kuongoza kikosi cha timu ya Taifa ya Denmark ambako ndiko alikozaliwa na kuishi.

Yusuph alizaliwa Juni 15, 1994 huko Copenhagen nchini Denmark, huku baba yake akiwa ni Mtanzania mwenyeji wa Mkoa wa Tanga, anayeitwa Shihe Yurary aliyekuwa akifanya kazi kwenye meli ya mizigo, ambayo ilikuwa ikifanya shughuli zake kati ya Afrika na Denmark, na mama yake anayejulikana kwa jina la Lene ni raia wa Denmark.

Kupitia kazi zake hizo, Shihe alikutana na Lene na kuanzisha uhusiano uliomleta duniani Yusuf,  na akaamua kuhamishia makazi yake jijini Copenhagen, Denmark ni raia wa  Denmark.

Yusuf alianza kucheza soka akiwa mdogo, na kujiwekea rekodi mbali mbali mpaka kusajiliwa na timu ya RB Leipzig ya nchini Ujermani, ambako bado yupo mpaka sasa.

Kwenye timu yake ya Taifa ya Denmark Yusuf anacheza nafasi ya mshambuliaji, ambayo ni maalum kwa kufunga magoli, na imetajwa kushiriki kombe la dunia mwaka 2018, ambaloi linatarajia kuanza siku si nyingi nchini Urusi.
 

Yussuf Yurary Poulsen