Jumatatu , 7th Jul , 2014

Msanii wa muziki wa kike wa miondoko ya Afro Pop nchini Vanessa Mdee aliyetwaa tuzo ya Kili Music kwa mwaka huu kwa wimbo wake 'Hawajui' yupo mbioni kufanya kolabo na kundi la Sauti Sol nchini Kenya.

Msanii wa muziki nchini Tanzania Vanessa Mdee

Vanessa Mdee ambaye hivi karibuni amefanya kolabo na wasanii wa kike nyota wa Kenya wakiwemo Victoria Kimani na Xtatic, ameelezea kuwa anajiandaa kuingia studio na kundi hilo litakaporudi likitokea nchini Amsterdam katika ziara ya muziki.

Hivi sasa dashosti huyo anafanya vyema na kichupa chake kipya cha wimbo wake 'Come Over' kilichotayarishwa na prodyuza Nahreel.