Ijumaa , 4th Jul , 2014

Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) nchini Tanzania limewataka wananchi kupuuza taarifa za upotoshaji ku

Wabunge Iddi Azzan na Zitto Kabwe (pichani) wakiwa kwenye moja ya mazoezi wakati walipohudhuria mafunzo yanayotolewa na Jeshi la Kujenga Taifa - JKT.

Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) nchini Tanzania limewataka wananchi kupuuza taarifa za upotoshaji kupitia mitandao ya jamii na simu za mkononi kuhusu kuwepo kwa mateso na vitendo vya ukatili kwa vijana wanaojiunga na mafunzo yanayoendeshwa na jeshi hilo.

Akizungumza jijini Dar-es-Salaam Msemaji wa Jeshi la Kujenga Taifa Emmanuel Muruga amekanusha uvumi huo unaodai kuwa vijana wanaoendelea na mafunzo katika kambi za JKT kwa mujibu wa sheria huwa wanakufa kwa ukatili na kusema jambo hilo ni uzushi na upotoshaji.

Hata hivyo Muruga amesema kwa sasa kuna idadi ya vijana wapatao 38,634 waliojitolea na waliopo kwa mujibu wa sheria na wanaendelea na mafunzo katika makambi yote.