Jumatano , 25th Jun , 2014

Tukio la ajali ya gari ambalo limeripotiwa kumhusisha msanii Bebe Cool katika barabara ya Entebbe, limetajwa kuwa ni mpango ambao umetengenezwa kwaajili ya kuvuta watu katika onyesho la “Best of Bebe Cool” litakalofanyika hivi karibuni.

Msanii Bebe Cool wa Uganda akiwa na mkewe Zuena

Kwa mujibu wa wachunguzi wa mambo, timu ya Bebe Cool imekuwa ikipanga tukio hili sambamba na mengine kadhaa kwa mwezi mzima, mpango ukiwa ni kutangaza kuwa staa huyu amepoteza fahamu na baadaye kuja kuzinduka siku chache kabla ya show.

Hakuna majibu yoyote kutoka kambi ya Bebe Cool mpaka sasa kwaajili ya kutoa ufafanuzi wa swala hili, na rekodi inaonyesha kuwa ni kweli wasanii wa Uganda wamekuwa na utaratibu wa kutengeneza matukio ili kuvuta mashabiki kufuatilia wanachokifanya.