Jumanne , 19th Dec , 2017

Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla ametengua uteuzi wa Wajumbe wa Bodi ya Mamlaka ya  Hifadhi Eneo la Ngorongoro.

Waziri Kigwangalla amefikia uamzi huo baada ya hivi karibuni Rais Magufuli kumteua Prof. Abiud Kaswamila kuwa Mwenyekiti Mpya wa Bodi.

Taarifa kutoka Wizara hiyo imeeleza kuwa uteuzi mpya wa wajumbe wa Bodi hiyo utafanyika hivi karibuni.
Taarifa ya Wizara.