
Hayo amesema leo Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dr. Anna Makakala.
''Hizo ni taarifa za kiuchunguzi ambazo bado tunaendelea nazo, huwezi kuweka wazi kila kitu wakati bado tupo katika uchunguzi, tunapokuwa na shaka na mtu yoyote kuhusu uraia wake tunaruhusiwa kumuhoji,'' amesema Dr. Makakala.
Madai ya Askofu huyo kuhusu kuhoji upatikanaji wa katiba mpya ndio sababu ya kuhojiwa na idara hiyo, Dr. Anna amekanusha na kusema wawaache kwanza hadi uchunguzi utakapokamilika.
''Hayo ya kwake, naomba tusubiri uchunguzi hadi utakapo kamilika,'' ameongeza