
Bi. Bupilipili ametoa agizo hilo katika kijiji cha Kunzugu alipokuwa anazungumza ikiwa ni siku ya maadhimisho ya siku ya Ukimwi wilayani humo, ambayo pia iliadhimishwa kwa kupanda miti.
Mkuu huyo wa wilaya amewataka polisi kupita nyumba kwa nyumba kwenye nyumba za wageni, na kuwasaka wanawake ambao wanadaiwa kukodisha nyumba hizo kwa ajili ya kuendesha biashara za ukahaba.