
Kauli hiyo ya Maaskofu imekuja baada ya mkutano wao kuthamini hali ya kisiasa nchini humo huku kukiwa na na shinikizo kutoka Jumuiya ya Kimataifa, kwa serikali ya DRC kuhakikisha uchaguzi huo unafanyika kama ilivyopangwa.
Hata hivyp hayo yanajiri wakati ambapo serikali ya DRC imepiga marufuku maandamano yaliyopangwa wiki hii kushinikiza kujiuzulu kwa Rais Joseph Kabila.
Uchaguzi Mkuu nchini DRC umepangwa kufanyika nchini humo mwezi Disemba mwakani wakati huo upinzani wa nchi hiyo umekuwa ukidai kuwa Kabila, anapanga kuwania tena kinyume cha katiba, madai ambayo Rais huyo bado hajajibu.