
Baadhi ya wanachama wa klabu ya Yanga
Klabu ya soka ya Dar es salaam Young Africans maarufu kama Yanga imewataka wanachama wa klabu hiyo kufuata kanuni na taratibu za katiba ya klabu hiyo, kwa lengo la kutowapa mwanya wapinzani na kusababisha migogoro isiyo na tija ndani ya klabu hiyo.
Mwenyekiti wa Matawi ya Klabu ya Yanga Mohamedi Aly amewaambia waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo kwamba mwanachama ambaye atakuwa na matatizo na klabu hiyo ni vema akayawasilisha kwa mwenyekiti wa tawi badala ya kuvunja sheria za klabu hiyo na kuchukua jukumu la kulipeleka tatizo hilo pasipo husika.
Amesema iwapo kila mwanachama atakuwa na uamuzi wa kuizungumzia Yanga bila ya kufuata taratibu jambo hilo linaweza kuleta mtafaruku ndani ya klabu na hivyo ni vyema kila mwanachama akafuata taratibu za klabu hiyo